5. Maana ya mofolojia
• Mofolojia ni tafsiri ya neon la kiingereza
“Morphology”. Neno hili nalo linatokana na
neon la kiyunani “Morphe” lenye maana ya
muundo au umbo ( Aurbach et al 1971; 106).
• Mofolojia ni neno linalotumiwa kumaanisha
utanzu wa isimu unaoshughulikia muundo wa
maneno ( Habwe na Karanja 2004).
6. Maana..........
• Hartman (1972). Mofolojia ni tawi la
sarufi ambalo hushughulika na uchunguzi
na uchambuzi wa maumbo, fani na aina
za maneno yalivyo sasa pamoja na
historia zake
7. Maana.........
• Kwa ujumla mofolojia ni taaluma
inayoshughulikia lugha pamoja na
mpangilio wake katika uundaji wa
maneno. Vipashio hivyo vya lugha
huitwa mofimu
8. Uhusiano uliopo kati ya mofolojia na
matawi mengine ya sarufi
• Mofolojia na fonolojia
• Kuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya
mofolojia na fonolojia:i. Vipashio vya kifonolojia ndivyo hutumika
katika kuunda vipashio vya kimofolojia
mfano
9. Mofolojia na fonolojia
• Vipashio vya mofolojia ni fonimu, mfuatano
wa fonimu ndio huuna vipashio vya
kimofolojia ambavyo ni mofimu
Mfano
• Fonimu: i, p, t, a, huunda
• mofimu: Pit-a
• Hivyo basi neno pita limeundwa na mofimu mbili na fonimu nne
10. Mofolojia na fonolojia
ii) Uhusiano mwingine kati ya fonolojia na
mofolojia ni kwamba, kanuni za kifonolojia
hutumika kueleza maumbo ya kimofolojia
ambayo yanaathiriana.
Mfano
Katika neno mu-ana
mwu-alimu
11. Mofolojia na fonolojia
• Kipashio [mu] katika mifano hapo juu
kinajitokeza kama [mw-] inapofuatwa na irabu
ambayo.
Mu
mw-/-I
12. Mofolojia na sintaksia
i. Vipashio vya msingi vya kimofolojia ndivyo
hutumika katika kuundia daraja hili la
sintaksia
Mfano
Neno hutumika kuundia sentensi